THAMANI YA SHAMBA LA MIPAINA/PINES HAIPO KWENYE WINGI WA MITI



 
Shamba la Miti ya Mipaina/Pines ambayo haijapunguziwa

Karibuni tena kwenye SmartForestry na leo naomba kuzungumzia kuhusu Thamani ya shamba la Mipaina/Pines katika kilimo cha kibiashara kwa kuangalia faida na hasara za kuwa na miti mingi shambani. Tunaongelea Mipaina zaidi kwa sababu ndio miti pekee inayotawala kwenye soko hasa la mbao kwa sasa, hivyo ubora na thamani yake ipo zaidi kwenye unene na urefu wa mti shambani.
Tukirejea kwenye maandiko yangu yaliyopita nimezungumzia kwa undani mbegu bora na upandaji miti, idadi gani ya miti inapaswa kupandwa shambani na umbali wa mti na mti unaopendekezwa. Unaweza rejea makala zangu zilizopita kwa maelezo zaidi.

“Naomba nikazie kwa kusema kuwa Thamani ya shamba la Mipaina/Pines haipo kwenye wingi wa miti shambani, kitu cha msingi kuzingatiwa ni kuhakikisha unapanda kwa umbali angalau mita 3x3(Ft9x9) na unapunguzia miti kila baada ya miaka mitano

Punguza angalau theluthi moja (1/3) ya miti iliyopo shambai kwako pale miti inapofikisha miaka 6 (sita) na kufanya hivyo tena pale miti inapofikisha umli wa miaka 11(kumi na moja) kwa kuhakikisha inabaki nusu ya miti iliyopandwa mwanzoni.

Mfano: Kama ulipanda miti 545 katika shamba lako la ukubwa wa mita 70x70. Baada ya miaka 5 unatakiwa kupunguzia miti angalau 150 ndani ya shamba lako na kubakisha miti 395. Hakikisha pia kwenye umli huu Upogoleaji/Pruning ya kwanza iwe imefanyika. Hapa itabidi upunguzie tena baada ya miaka mitano mingine kwenye umli wa miaka 11 kwa kupunguza miti angalau 120 ili ibaki miti 275 ndani ya shamba ambayo itavunwa kwa faida kubwa zaidi.

FAIDA ZA KUPUNGUZIA MITI

Kupunguzia miti (Thinning) katika shamba la miti ni zoezi la kuondoa baathi ya miti na kuacha mingine ili kuipa nafasi nzuri ya ukuaji. Na mara nyingi inafanyika kwenye shamba la miti kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa sita kwa kuondoa miti ambayo ni migonjwa au ile inayokuwa kwa kupinda. Miti ilioachwa baada ya kupunguza mingine hukua kwa haraka kwa kupata zaidi mwanga wa jua na hewa pamoja na kuipunguzia urefu wa seli bomba za mti (Tracheids) ambazo zina kazi ya kupitisha maji pamoja na  virutubisho kwa ukuaji wa mti.

Pia hupunguza athali za wadudu waharibifu kwenye ngozi ya mti (Dendroctonus adjunctus), zoezi hili pia hupunguza madhala ya moto kwenye shamba na huongeza kiwango cha uozaji wa majani ya miti kwa ajili ya kurutubisha ardhi.

Biashara ya mbao kwa miti iliyopunguzwa kwenye mwaka wa sita itaweza kukupatia fedha kwa ajili ya matunzo ya mashamba yako ya miti na kukuongezea kipato kabla ya uvunaji wa mwisho. Hivyo sio maamuzi sahihi kuvuna miti yako yote kabla haija komaa na yenye kukupa hasara.

Matokeo muhimu ya kupunguzia miti ni kuongeza ujazo/ukubwa na thamani ya kibiashara kwa mti mmoja mmoja ndani ya shamba la miti ambapo miti hurefuka zaidi na kutanuka zaidi kuwa na kipenyo (Diameter) kikubwa chenye kutoa mbao bora na zenye thamani kubwa. Ambapo unaweza kuuza mti mmoja kwa zaidi ya TSh. 100,000/ na zaidi.

Comments

  1. upandaji wa miti ya mipaina inacost shs ngap kwa muda gani na mtaji wake ni shs ngapi

    ReplyDelete
    Replies
    1. @noela Jaribu kutembelea huu ukurasa wa facebook kuna jedwali rahisi la mchanganuo wa ghalama za uanzishaji shamba la miti pamoja na mapato yake. Kama kutakuwa kuna swali usisite kunitumia hapa au kule facebook.

      https://web.facebook.com/smartforestry/photos/a.1990152764584364/1992204097712564/?__cft__[0]=AZXZXomgX1qOZwnFeJWFcdXZ5i8gCca-8YtG1uQzJC7HewjqsRWagUdgNuu6z_XMQbnV-P_TGsj8fJlap6wZBXIex8pFw16GEZXUxPidgRrrBs0wg9HNAiANvy-_gW0DPr3uZpBviVqaJXxFqtJ3fREP6_S-ePoQQbQxRfJcdKUU-gjyGpeZF-Maj1SgiwFafnM&__tn__=EH-R

      Delete
    2. Mipaina inawezekana kustawi kwenye maeneo ya mwambao wa ziwa

      Delete
    3. Nimejaribu kuifuata hiyo link lakini naona haifunguki. FB unatumia jina hilo hilo!?

      Delete
  2. Naomba kuuliza maswali na naomba unijibu kwa gmail au no 0688424929

    Je Mipaina lazima usihe mbegu ndipo upande au unaweza kuandaa shamba na ukapanda mbegu kwa kutumia mbolea ilizikue moja kwa moja ? Na jee nawezaje kupata mbegu hizo za Mipaina na kwa bei gani?

    Kwasababu nipo kagera wiraya ya ngara nawezaje kufikiwa na mbegu hizo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uko ngara sehemu gani? Nina shamba huko

      Delete
    2. Kwa mbegu za mipaina, haiwezekani kusia/kupanda moja kwa moja shambani. Ndio mbegu zinapatikana kwa bei ya Ths 100,000 kwa kilomoja kwa mbegu/kimbo. Ndio unaweza kutumiwa.

      Delete
  3. Mipaini huchukua miaka mingapi toka kupandwa hadi kukomaa na kuvunwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kitaalamu ni miaka 18 hadi 20 ila kama ikitunzwa vizuri uvunaji unaweza kuleta faida baada ya miaka 10 tu.

      Delete
  4. Naomba kujua he mipaina inauwezo was kuhimili sehemu yenye Mani mengi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aina nyingi za mipaina zahiwezi ingawa kuna aina kama mbili ndio hasa zinaweza kuhimili ingawa inaweza kuwa shida kidogo kupata mbegu zake.

      Delete
  5. Ukipanda pines je inachukua muda gani kuanza kupruni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa kawaida ni kuanzia mwaka wa TATU hadi WANNE ingawa mara nyingi hutegemea zaidi na ukuaji wake.

      Delete
  6. naona wadau wanachat bila kujibiwa , ok any way , why no any reply?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Miti ya paini hichukua takribani miaka 8-10 kuvunva

      Delete
    2. Miti ya paini hichukua takribani miaka 8-10 kuvunva

      Delete
    3. Pole sana mdau kwa kuwa kimya.

      Nashukuru Salum.

      Delete
  7. Habar nipo Kanda ya ziwa naomba kuuliza pines imekua nashida Sana kipindi ipo kwenye kiriba inaweka njano na kukauka pale kwenye kichwa Cha mche naombeni nisaidienii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana kwa tatizo hilo, mara nyingi kwa dalili hizo huwa ni ukosefu wa virutubisho kutoka kwenye udongo au wadudu wanaotokana na mbolea(kama unatumia ya mboji) au udongo. Hivyo ni vyema ukabadilisha mchanganyiko wa udongo wakati wa kusia. Kama kuna jingine nipigie 0758116818.

      Delete
  8. Mimi na miti kama 150 ya mipaini imekomaa naitaji kuuza no 0788327959

    ReplyDelete
  9. Replies
    1. Habari yako Rajabu,
      Samahani nafikiri swali lako sijafanikiwa kulisoma, please nicheck kwenye 0758116818. Asante.

      Delete
  10. Ni miti gani hutumika kutengeneza karatasi? Je mipaina ina soko nje ya nchi yetu? Taja kwa uchache

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa Tanzania mipaina kwa muda mrefu imekuwa ikitumika zaidi ingawa miti kama milingoti na migrevilea hutumika pia. Ndio mipaina ina soko kubwa nje ya nchi hasa nchi ya Kenya, Zambia, Visiwa vya Comoro na nchi nyingine nje ya bara la Africa kwa mazao ya mbao pamoja na bidhaa za kuchakatwa kama Plywood na nyinginezo.

      Delete
  11. Mbegu zinapatikana?
    Naweza pataje Niko mkoa wa mwanza

    ReplyDelete
  12. Ndio mkuu zinapatikana, tuwasiliane 0758116818 kwani unaweza kutumiwa kupitia usafiri wamabasi ya mikoani.

    ReplyDelete
  13. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  14. Ivi kanda ya ziwa MWANZA inakubali

    ReplyDelete
    Replies
    1. Karibu sana, ndio inastawi vizuri, Nafikiri umeshasikia shamba la miti la Biharamuro, Chato? Pia maeneo toka Geita hadi karibu na Sengerema kuna hali ya mvua na udongo mzuri kwa kilimo cha Mitibiashara. Pia kwenye visiwa vya Ukerewe ipo Mitibiashara.

      Delete
  15. Nina shamba la miaka 10 ekari moja bei gani

    ReplyDelete
  16. Karibu sana Smart Agroforestry. Kwa kawaida thamani ya miti shambani hutegemea zaidi ukubwa wake (Diameter) pia na ubora wa mti (Straightness) kwenye kunyooka. Hivyo ni vyema nikaona angalau picha au kufika shambani.

    ReplyDelete
  17. Paine na karitusi ipi Ina soko zaidi

    ReplyDelete
  18. Kiongozi kuna miti ya mitiki iko sokoni, sasa kuna namna ambayo unaweza kunisaidia tupate connection ya soko!? Whatsapp 0742716837

    ReplyDelete
  19. kusiha mbegu mpaka zichipue inachukua muda gani na gharama kiasi gani?

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

USIYOYAJUA HUHUSU KILIMO CHA MITI

UWEKEZAJI BORA KWA MAZAO BORA YA MITI