KWANINI UWEKEZE KWENYE SEKTA YA MISITU?
Kuna fursa iliyopo ya uwekezaji katika sekta ya misitu na msukumo wa ukuaji wake endelevu, unaowahakikishia wakulima wadogo na wakubwa kutumia fursa shindanishi katika biashara ya mbao, nguzo, mirunda na nishati katika kujenga uboreshaji wa uchumi, mazingira, na jamii. Yafuatayo ni mambo MATANO muhimu kuzingatiwa katika uwekezaji katika sekta ya misitu; 1 Mahitaji ya Miti Kuongezeka. Kufikia mwaka wa 2030, mahitaji ya mbao yataongezeka kwa mara mbili ya hali ya sasa na yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku kwa sababu misitu kupungua, maendeleo ya bidhaa za misitu na idadi ya watu inazidi kuongezeka. Hata hivyo hadi sasa mahitaji ya nishati na karatasi bado kwa kiasi kikubwa yanategemea mazao ya miti. 2 . Bei ya Miti Kuongezeka Zaidi. Kuadimika kwa mazao ya misitu sokoni kama vile mbao, nguzo, mirunda, kuni na bidhaa nyingine za miti kunapanua fulsa ya biashara na thamani ya uwekezaji katika sekta ya misitu nchini. Mti huongezek...