USIYOYAJUA HUHUSU KILIMO CHA MITI
Tree Farmers from Sapanda village in Ileje sells the unpotted Pines seedlings in Isangati village in Mbeya rural, Feb2015. Kilimo cha miti kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania, Mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa. Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea nyumba na utengenezeaji wa karatasi. Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambako mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa (carbon dioxide). Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo au miti ghafi ya kutengenezea karatasi. Binafsi niliichangamkia biashara hii miaka minne iliyopita na 'I'm real serious with it'. Nimejiwekea lengo la kupanda ekari 20 kila mwaka...