Posts

Showing posts with the label uwekezaji

UWEKEZAJI BORA KWA MAZAO BORA YA MITI

Image
Uwekezaji Bora. Uwekezaji wa kupanda miti unachukua muda mrefu kidogo ukilinganisha na mazao mengine ya nafaka hivyo toka muda wa kupanda inaweza kuchukua si chini ya miaka minne kwa Mikaratusi/Milingoti/Eucalyptus na miaka nane hadi kumi kwa Mipaina/Pines ndiyo uanze kuvuna. Unatakiwa kwenda nayo taratibu hivyo kila mwaka unaweza kupanda miti kiasi/heka chache ili utakapoanza uvunaji uendelee kuvuna kila mwaka na kupanda tena ulikovuna. NB: Lakini pia hili linategemea na malengo binafsi au kulingana na kipato cha uwekezaji. Kuhusu gharama za kununua na kupanda Miti zinatofautiana kufuatana na sehemu/mahali husika. Lakini kichocheo kikubwa huwa ni miundombinu na hali ya hewa nzuri kwa ustawi wa Miti. Kwa wakati huu maeneo mengi yenye rutuba na miundombinu nzuri yamepata wateja wengi na kupelekea wamiliki kupandisha bei ya Ardhi katika miaka ya hivi karibuni. Bei ya hekali moja kwa sasa inaanzia TSh 70,000/= kwa maeneo yaliyo mbali zaidi lakini inafika hadi 300,000/= kwa...