THAMANI YA SHAMBA LA MIPAINA/PINES HAIPO KWENYE WINGI WA MITI
Shamba la Miti ya Mipaina/Pines ambayo haijapunguziwa Karibuni tena kwenye SmartForestry na leo naomba kuzungumzia kuhusu Thamani ya shamba la Mipaina/Pines katika kilimo cha kibiashara kwa kuangalia faida na hasara za kuwa na miti mingi shambani. Tunaongelea Mipaina zaidi kwa sababu ndio miti pekee inayotawala kwenye soko hasa la mbao kwa sasa, hivyo ubora na thamani yake ipo zaidi kwenye unene na urefu wa mti shambani. Tukirejea kwenye maandiko yangu yaliyopita nimezungumzia kwa undani mbegu bora na upandaji miti, idadi gani ya miti inapaswa kupandwa shambani na umbali wa mti na mti unaopendekezwa. Unaweza rejea makala zangu zilizopita kwa maelezo zaidi. “Naomba nikazie kwa kusema kuwa Thamani ya shamba la Mipaina/Pines haipo kwenye wingi wa miti shambani, kitu cha msingi kuzingatiwa ni kuhakikisha unapanda kwa umbali angalau mita 3x3(Ft9x9) na unapunguzia miti kila baada ya miaka mitano ” Punguza angalau theluthi moja (1/3) ya miti iliyopo shambai kwako pale